Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern yabanwa mbavu na Salzburg

Bayern Salz Salzburg imekwenda sare ya magoli 1-1 na Bayern

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RB Salzburg imetoshana nguvu na Bayern Munich katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora mchezo uliopigwa Jumatano usiku na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Salzburg wakiwa kwenye ubora mkubwa kwenye mechi hiyo hasa kipindi cha pili walitangulia kupata goli kupitia shambulizi la kujibu ambalo limefungwa na Chukwumbuike Adamu akimalizia pasi ya Brenden dakika ya 21.

Wakati Bayern Munich ambao ni vinara wa Bundesliga bao lao limefungwa na winga hatari Coman akimalizia mpira wa kichwa wa kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani Thomas Muller kunako dakika ya 90.

Bayern Munich itahitaji kushinda ili kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uefa, hata hivyo kama Salzburg watakuwa na ubora kama wa mechi ya Leo basi Munich watakuwa kwenye wakati mgumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live