Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern wamuwinda golikipa bora Kombe la Dunia

Emiliano Martinez Bayern Emiliano Martinez

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Aston Villa aliyeshinda Kombe la Dunia Emiliano Martinez anasakwa na wababe wa Ujerumani Bayern Munich iliyopo chini ya kocha mkuu Julian Nagelsmann.

Ingawa Lionel Messi ameshikilia vichwa vya habari kwa nafasi yake katika ushindi maarufu wa Argentina baada ya kumtungua Ufaransa kwa mikwaju ya penalti 4-2.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye alishawahi kutolewa kwa mkopo timu kama Oxford, Sheffield Wednesday na Rotherham.

Kando na hayo golikipa huyo katika dakika za lala salama dhidi ya Australia na Ufaransa, Martinez alikuwa shujaa wa mikwaju miwili ya penalti dhidi ya Uholanzi na Les Bleus kwa kuokoa mikwaju ya penalti.

Bayern wanatamani sana kuimarisha safu yao ya walinda mlango msimu huu wa baridi baada ya Manuel Neuer kuvunjika mguu katika safari ya baada ya Kombe la Dunia kufanya vibaya.

Ingawa itakuwa ngumu kwa Muargentina huyo kukataa soka ya Ligi ya Mabingwa, Villa hawana shinikizo la kumuuza na nambari yao ya 1 wamepewa kandarasi hadi msimu wa joto wa 2027.

Bado wakala wa mchezaji huyo Gustavo Goni amebatilisha uvumi huo na baadhi ya maoni ya kutiliwa shaka kwa vyombo vya habari vya Italia mwishoni mwa wiki. Alipoulizwa kama mteja wake atafikiria kuhamia Serie A, Goni alijibu: “Leo kuna timu chache ambazo zinaweza kumudu kipa kama yeye.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live