Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern wamtega Alonso, apandishiwa Mshahara mara nne

Xabi Alonso .jpeg Kocha wa Bayern Liverkusen, Xabi Alonso

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bayern Munich inajiandaa kuvunja benki ili kuwapiku Liverpool kwenye mchakato wa kumnasa kocha Xabi Alonso.

Miamba hiyo ya Allianz Arena imepanga kumpa Alonso mshahara wa Pauni 20 milioni (Sh 64.6 Bilioni) kwa mwaka kama mshahara wake ili kumshawishi aondoke Bayer Leverkusen mwishoni mwa msimu huu wakati wao pia watakapomfungulia mlango wa kutokea Thomas Tuchel.

Jambo hilo litamfanya Alonso kuwa kocha anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwenye historia ya Bundesliga na kulingana na kocha anayelipwa mkwanja mkubwa zaidi kwenye Ligi Kuu England, Pep Guardiola.

Licha ya kwamba Alonso, 42, haonekani kufanya pesa kuwa kipambele chake, lakini mkwanja huo mrefu kama ofa aliyopewa huko Bayern inaweza kuikata maini Liverpool, ambayo pia itahitaji huduma ya kocha huyo kutokana na kuondokiewa na Jurgen Klopp mwishoni mwa msimu huu.

Leverkusen haijapoteza mchezo wowote kwenye michuano yote msimu huu. Huko kwenye kikosi cha Leverkusen, Alonso analipwa mshahara wa Pauni 5 milioni kwa mwaka. Hiyo ni nusu ya kiwango ambacho Tuchel analipwa huko Bayern.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live