Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern waendelea kukomaa na Harry Kane, waomba kikao

Harry Kane.jpeg Harry Kane

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabosi wa Bayern Munich bado hawajakata tamaa kwenye mpango wa kuipata huduma ya Harry Kane na kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya kufanya mkutano mwingine na mwenywekiti wa Tottenham Hotspur Daniel Levy juu ya staa huyo.

Mabingwa hao wa Bundesliga tayari wameshuhudia ofa zao mbili zikikataliwa na Spurs juu ya Kane, ambaye mkataba wake unamalizika mwakani.

Hadi sasa Tottenham haijataja bado bei ya fundi huyu kwani bado wana imani kwamba wanaweza kumshawishi asaini mkataba mpya.

Levy alikutana na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Bayern Jan-Christian Dreesen mapema Julai, lakini mwenyekiti huyo wa Spurs hakuonyesha dalili ya kuwa tayari kumuuza Kane na alisisitiza kwamba bado wanamhitaji kwenye timu na watapambana kumsainisha mkataba mpya.

Hata hivyo mbali ya msimamo huo wa Levy kwenye kikao cha kwanza, vigogo wa Munich wamepanga kukutana naye tena ili kuona ikiwa wanaweza kumshawishi akubali kumuachia straika huyo.

Inaelezwa kwamba C.EO wa Munich, Dreesen na mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Marco Neppe hawakusafiri na timu kwa ajili ya ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya barani Asia na badala yake wataenda kukutana na Levy na kufanya naye mazungumzo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live