Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern kuibomoa Chelsea kwa Mateo Kovacic

Mateo Kovacic .jpeg Mateo Kovacic

Sat, 29 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Klabu Bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Thomas Tuchel amemfanya kiungo wa Chelsea, Mateo Kovacic kuwa chaguo lake la kwanza kwenye usajili ujao wa dirisha kubwa.

Kovacic amekuwa na maisha magumu ndani ya Chelsea kwa msimu huu akianza michezo 15 pekee kati ya 33 za timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya England huku akitajwa kuwa moja ya wachezaji ambao wataonyeshwa mlango wa kutokea baada ya msimu kuisha.

Kwa mujibu wa mtandao wa Sport1 wa Ujerumani umeeleza kuwa Kovacic ni moja ya wachezaji ambao wataondoka ndani ya timu hiyo kutokana na upana wa kikosi cha timu hiyo huku nafasi yake ikiwa haba.

Kutokana na hilo, Tuchel anataka kumsajili kiungo huyo kwa kuwa anaamini kuwa na kiwango katika eneo anaweza kuifanya timu yake la kiungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live