Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern hawakamatiki, Barca yajitutumua

Bayern Sane Mshambuliaji wa Bayern, Leroy Sane ambae amefunga magoli mwawili kwenye mchezo huo

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa Oktoba 20, Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo katika kundi E vigogo wa Soka kutoka nchini Ujerumani walisafiri mpaka nchini Ureno kwenda kuvaana na Benfica.

Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Luz Jijini Lisbon, umeshuhudia Benfica wakipigwa kipigo cha magoli 4-0 na Bayern Munich.

Mabao ya Bayern Munich yamefungwa na Leroy Sane mawili dakika ya 70 na 84, Éverton aliyejifunga dakika ya 80 na Robert Lewandowski dakika ya 82.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, hatimaye ilishuhudiwa Barcelona ikipata ushindi wake wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Dynamo Kiev 1-0, bao pekee la mlinzi Gerard Pique katika Uwanja wa Camp Nou.

Kwa pointi hizo tatu za kwanza baada ya mechi tatu, Barcelona inayofundishwa na kocha Ronald Koeman inapanda nafasi ya tatu, mbele ya Dynamo Kiev yenye pointi moja na nyuma ya Benfica yenye pointi nne na vinara, Bayern Munich wenye pointi tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live