Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern Munich yashikwa shati na Cologne

Bayern Vs Cologne Bayern Munich yashikwa shati na Cologne

Wed, 25 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vinara wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bayern Munich wamepambana na kupata alama moja kwenye mechi ya Ligi dhidi ya Cologne huku kiraka Joshua Kimmich akiibuka mwokozi wa ng’ambo kwa kufunga bao la kusawazisha dakika za lala salama.

Cologne wakishika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi baada ya michezo 17 waliweza kuitangulia Bayern kufunga kunako dakika ya nne tu bao likifungwa na Ellyes Skhiri.

Pamoja na kutawala mchezo kwa ujumla wake, Bayern walilazimika kusubiri mpaka dakika ya 90 kutupia bao hilo.

Kwa matokeo hayo, Bayern inaendelea kuwa kileleni kwa tofauti ya pointi nne ya RB Leipzig ambao walikwea mpaka nafasi ya pili kufuatia kuichapa 6-1 Schalke 04.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live