Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern Munich yamtaka Onana

Amadou Onana Everton 5860237 Amadou Onana

Thu, 27 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bayern Munich imeweka wazi dhamira yake ya kunasa saini ya kiungo Amadou Onana, lakini klabu yake ya Everton inataka Pauni 50 milioni.

Kocha mpya wa Bayern Munich, Vincent Kompany atahitaji kumvuta Mbelgiji mwenzake huko Allianz Arena kwenda kuongeza nguvu kwenye sehemu ya katikati ya kikosi hicho cha miamba ya Bundesliga.

Everton imefungulia mlango wa kumpiga bei Onana, 22, wakati huu ikitaka pesa ili kwenda sawa na kanuni za mapato na matumizi za Ligi Kuu England.

Hata hivyo, haipo tayari kumuuza kwa bei ndogo ikihitaji kupata faida kwa mchezaji huyo aliyenaswa kutoka Lille kwa ada ya Pauni 30 milioni miaka miwili iliyopita.

Kocha wa Everton, Sean Dyche hakumtumia Onana kwenye mechi chache za mwishoni mwa msimu uliopita na hilo linaonyesha wazi miamba hiyo ya Goodison Park ipo tayari kumuuza Mbelgiji huyo kuliko beki Jarrad Branthwaite anayewindwa na Manchester United.

Mchezaji aliyepangwa kuziba pengo la Onana ni mkali Iliman Ndiaye ambaye atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na kocha Dyche kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 24 ataigharimu Everton Pauni 15.3 milioni atakaponaswa kutoka Marseille na tayari makubaliano binafsi yameshafikiwa. Atakapotua huko Merseyside atakwenda kuungana na staa wa Pauni 9 milioni, Tim Iroegbunam, aliyenaswa kutoka Aston Villa na winga Jack Harrison — ambaye atatumikia msimu wake wa pili kwa mkopo kwenye kikosi hicho akitokea Leeds United.

Ashley Young ameungana na veterani mwenzake Seamus Coleman, 35, ambao wamesaini mikataba mipya ya mwaka mmoja kubaki Goodison Park.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live