Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayern Munich kuinufaisha The Three Lion

Skysports Harry Kane Bayern Munich 6265178 Bayern Munich kuinufaisha The Three Lion

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya England Gareth Southgate anaamini kuwa timu yake inaweza kufaidika kutokana na uhamisho wa Harry Kane kwenda Ujerumani, haswa ikiwa nahodha wake huyo atajinyakulia taji la kwanza katika maisha yake ya soka akiwa Bayern Munich.

Kane mwenye umri wa miaka 30, aliondoka katika klabu yake ya utotoni, Tottenham Hotspur na kutimkia Allianz Arena kwa mkataba ambao uligharimu Pauni Milioni 100.

Alikuwa akihusishwa na kuondoka Spurs kwa misimu michache iliyopita, sasa mustakabali wa Kane na Southgate anafurahi kumuona akikipiga akiwa Bayern.

“Kwa hakika nafikiri kwa mtazamo wangu ni vema hatima yake iwe imetulia sasa kwa miaka michache ijayo,” alisema kocha huyo wa England.

“Nadhani uwezekano huo unaweza kuwa usumbufu kwa wachezaji. Lakini ni vizuri kwake kwamba lazima aende kucheza katika klabu mpya. Amekuwa kwenye klabu moja kwa muda mrefu.

“Kuwa na mabadiliko inamaanisha lazima ufurahie wachezaji wenzake wapya, wafanyakazi wapya, mashabiki wapya na pia kuna uzoefu wa maisha na kuzoea nchi mpya. Nadhani kuna mazuri mengi huko.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live