Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya wenyeji Bayern Munich na Barcelona, Rais wa klabu ya Bayern Markus Soder amesema mchezo huo utachezwa bila mashabiki ikiwa ni sehemu ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Covid-19.
Bayern Munich watacheza na Barcelona Disemba 8, 2021 katika mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi, kipindi ambacho wenyeji Munich tayari imeshafuzu wakati Barcelona na Benfica bado mambo hayajakawa sawa.
Barcelona wanahitaji ushindi kufuzu hatua ya 16 bora Wakati Benfica wanahitaji ushindi lakini wakati huo huo kuwaombea Barca kukalia msumali.
Benfica watacheza na Dynamo Kyiv muda na siku moka ambayo Bayern Munich watacheza kuepuka upandaji wa matokeo.
Barcelona walipoteza mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Bayern Munich kwa bao 3-0, mara ya mwisho kushinda Allianz arena mara ya mwisho ilikuwa Machi 2015.