Basi la timu ya Sofapaka FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya, limepigwa mnada ili kufidia malimbikizo ya mishahara ya wachezaji wa zamani wa klabu hiyo.
Michael Kibwage na Paul Kiongera waliiomba Mahakama ya Kibiashara nchini Kenya ipige mnada Basi hilo ili kukamilisha mpango wa kulipwa malimbikizo ya mishahara waliyokuwa wanaidai Klabu hiuyo ambayo imewahi kutwaa Ubingwa wa nchini Kenya.
Taarifa kutoka Kenya zinaeleza kuwa Basi hilo limepigwa mnada kwa Shilingi Milioni moja, na wakati wowote wachezaji Michael Kibwage na Paul Kiongera watalipwa sehemu ya fedha hizo zilizopatikana.
Hii ni mara ya pili kwa mchezaji kupiga mnada Basi la klabu hiyo baada ya Wellington Ochieng kufanya hivyo hivyo mnamo Machi 2023 kufuatia madai yake kwenye klabu ya Gor Mahia.