Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basi la Lyon lashambuliwa, Kocha ajeruhiwa

Lyon Basi la Lyon lashambuliwa, Kocha ajeruhiwa

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo wa Ligue 1, kati ya Olympique Marseille dhidi ya Olympique Lyon umeahirishwa baada ya basi la Lyon kushambuliwa kwa mawe na matofali kabla ya mchezo huo na kupelekea majeraha kwa kocha mkuu wa Lyon, Fabio Grosso.

Shambulio hilo limepelekea kocha huyo raia wa Italia kuvuja damu nyingi kutokana na vipande vya kioo kumpiga usoni baada ya mawe kurushwa kwenye basi hilo kabla ya mchezo kati mahasimu hao wakubwa wa Ligi Kuu Ufaransa.

Tukio hilo lilitokea wakati klabu hiyo ikitoka katika hoteli yao kuelekea katika dimba la Velodrome kwa ajili ya pambano lao na Marseille siku ya Jumapili. Kocha msaidizi wa Lyon pia ameripotiwa kujeruhiwa.

Sio mara ya kwanza kwa matukio ya vurugu kujitokeza kabla au wakati wa mechi za Olympique Marseille.

Itakumbukwa mwezi uliopita polisi wa kutuliza ghasia walikumbwa na mlipuko wakati mashabiki wa Marseille na Ajax walipopambana nje ya uwanja wa Johan Cruyff Arena kabla ya mchezo kati ya vilabu hivyo.

Kwa mujibu wa ripoti Mashabiki 12 wa Marseille walikamatwa - sita kwa kubeba silaha za hatari huku wengine sita wakiripotiwa kukamatwa kwa kuzurura.

Mwaka jana Mashabiki wa Tottenham Hotspur walipata mapokezi mabaya kutoka kwa mashabiki wa Marseille kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mnamo Oktoba 2021, mshambuliaji wa PSG, wakati huo Neymar Jr alikumbwa na kadhia ya aina hiyo baada ya mashabiki kumtupia chupa tupu za plastiki, vikombe na vipande vingine vya takataka ili kumvuruga Mbrazil huyo wakati wa pigo la mpira wa kona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live