Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashungwa: Vyama vya michezo tumieni Taifa Cup

Inno Bash Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent l. Bashungwa

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: Dar24

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent l. Bashungwa ametoa wito kwa vyama vya kitaifa vya michezo, kutumia mashindano ya Taifa CUP 2021 kuchagua vipaji vya wachezaji na kuviendeleza ili kupata vipaji vitakavyounda timu za Taifa za michezo mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo, leo Desemba 10,2021 wakati alipokuwa akifungua mashindano ya Taifa CUP 2021 kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania, wanashiriki kikamilifu katika shughuli za michezo kwa kuwa michezo inatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi hususan kwenye Marnie ya uchumi, siasa na jamii.

“Kimsingi michezo ni ajira, amani, mshikamano, afya na furaha. Kutokana na umuhimu huu wa sekta ya michezo, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeamua kwa dhati kabisa, kwa kusaidiana na Vyama vya Michezo chini ya Baraza la Michezo la Taifa, kuanzisha shindano la Taifa Cup ambalo lilikuwa halipo kwa miaka kadhaa”. Amefafanua Waziri Bashungwa.

Chanzo: Dar24