Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basena ameacha ujumbe mzito Ihefu FC

Basena Ihefu.png Basena ameacha ujumbe mzito Ihefu FC

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Pamoja na kumtimua Kocha Moses Basena, Ihefu FC inafikisha idadi ya makocha watatu hadi sasa kuachana nao ikiwa ni zaidi ya mechi walizoshinda kwenye mechi 12 ilizocheza kwenye Ligi Kuu.

Ihefu ilianza na John Simkoko aliyedumu kwa mechi mbili akimuachia kijiti Zuberi Katwila ambaye naye aliiongoza mechi nne kisha kutimkia Mtibwa Sugar na kumleta Basena raia wa Uganda aliyesimamia michezo saba.

Basena katika mechi saba alizosimamia timu hiyo, amepoteza mechỉ tatu na sare nne na kuiacha nafasi ya 14 kwa pointi 10 baada ya michezo I2 iliyocheza kwa ujumla akiwa hajawahi kupata ushindi na timu hiyo.

Mbali na makocha, timu hiyo imeonekana kuwa mwiba mkali kwenye vyeo vingine kwani kabla ya kumtangaza Biko Scanda kuwa mtendaji mkuu, alitangulia Muhibu Kanu ambaye wameachana kimyakimya.

Baada ya kuondoka klabuni hapo Kocha Basena amesema licha ya matokeo kuhusika kwenye uamuzi huo, lakini bado alikuwa na uwezo wa kuibadili timu hiyo kutokana na kikosi alichokikuta.

Amesema hajahusika na usajili, lakini hata wachezaji hawana ubora kutokana na wengi kutumika kwa muda mrefu, hivyo alitarajia dirisha dogo kukisuka upya.

“Wachezaji wote nimewakuta na wengi ni kama wamechoka, mimi siyo mganga wa kienyeji japokuwa nilikuwa nasubiri Dirisha Dogo nifanye maboresho, lakini nakubaliana na walichoamua,” amesema Basena.

Chanzo: Dar24
Related Articles: