Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barua ya Dani Alves yazua gumzo

Alves Letter Dani Alves na aliyekuwa mkewe, Joana Sanz

Sat, 25 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Barua ya beki, Dani Alves aliyomwandikia aliyekuwa mke wake Joana Sanz imefichuliwa lakini beki huyo akiendelea kusota jela kufuatia kesi ya ubakaji inayomkabili.

Beki huyo wa zamani wa Barcelona, aliandika barua hiyo akiwa jela ya ‘Brian 2’ iliyopo Hispania akishikiliwa kwa mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia.

Imeelezwa Alves aligoma kula baada ya mwanamitindo huyo kutangaza rasmi ameachana na mwanasoka huyo kutokana na madai yanayomkabili.

Alves anakabiliwa na kesi ya kumshambulia mwanamke bafuni kabla ya kumbaka, baadaye mwanamke huyo ambaye hakufahamika jina alimripoti polisi na kukamatwa, tukio hilo lilitokea Desemba 31 mwaka jana.

Nyota huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Brazil, alichanganyakiwa baada ya ndoa yake kuvunjika kwa mujibu wa ripoti. Spanish TV ilisema barua hiyo imefichuliwa baada ya Joana kutangaza rasmi ndoa yake na beki huyo imevunjika rasmi kupitia akaunti yake ya Instagram.

Hii hapa barua ya Alves aliyomwandikia aliyekuwa mke wake

“Kipenzi changu Joan, imepita miaka minane sasa ya upendo wetu na heshima. Miaka ya nyuma mambo yetu yalikuwa mazuri na yenye furaha, wewe na watoto wangu (Dani Filho na Victoria), Tumekua pamoja tangu siku tulionana, tumeongozana pamoja kwa jambo lolote, tulipitia magumu mimi na wewe, nasikitika umeivunja ndoa yetu, nitaomba kila siku unipe nafasi nyingine ya kukupenda tena, naelewa maumivu unayopitia, nitaendelea kupambana kwa ushirikiano wa familia yangu, ukweli utagundilika na dunia itafahamu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live