Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bares: Kila mtu ashinde nyumbani kwake

Abdallah Baresi Angalizo Bares: Kila mtu ashinde nyumbani kwake

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union kocha mkuu wa Mashujaa, Abdallah Mohammed ‘Bares’ amesema kila mtu ashinde kwake.

Kipigo dhidi ya Coastal Union ni cha pili kwa Mashijaa baada ya kukandwa na JKT Tanzania bao 1-0, zote ugenini na sasa wanaialika Azam FC nyumbani kwao ambapo wana rekodi nzuri ya matokeo.

Timu hiyo hadi sasa kwenye mechi sita walizocheza wameshinda mechi mbili nyumbani suluhu moja ugenini dhidi ya Namungo na vipigo viwili.

Akizungumza na Mwanaspoti, Bares alikiri kuzidiwa uwezo na Coastal Union huku akiweka wazi kuwa kila timu ishinde mechi za nyumbani kwake na kuwaonya Azam FC ambao wa nakutana nao Nombemba Mosi kuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani hawana cha kupoteza.

“Tulizidiwa uwezo na Coastal Union ndio maana tumekubali kichapo hicho nimeona makosa ya wachezaji wangu nitayafanyia kazi kabla ya kuvaana na Azam FC kwenye uwanja wangu wa nyumbani;

“Hatutakuwa na cha kupoteza tutapamba kuhakikisha tunatumia vyema uwanja wa nyumbani kukusanya pointi tatu hilo halitushidi kutokana na rekodi nzuri tukiwa uwanja wa nyumbani.” alisema.

Bares alisema licha ya kuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wataingia kwa kuwaheshimu wapinzani wao kwa kusawazisha makosa waliyofanya mchezo uliopita.

Chanzo: Mwanaspoti