Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona yasuka akili kumpata Nico Williams

Nico Williams Barca Nico Williams

Fri, 19 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Katika kuhakikisha mambo hayaharibiki, Barcelona kwanza imeanza kufanya mazungumzo na wawakilishi wa winga wa Athletic Bilbao, Nico Williams kwa ajili ya kufanya nao makubaliano binafsi kabla hawajaendelea kuzungumza na Bilbao kuiomba ikubali kuwauzia mchezaji huyo.

Barca inataka kumalizana na Nico katika ishu ya maslaji binafsi kwa sababu inahofia timu za England zisiingilie kati na kuharibu mambo.

Wakala wa staa huyu alikutana na Mkurugenzi wa Ufundi wa Barcelona jana kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kukubaliana maslahi binafsi katika kikao ambacho kilifanyika huko Zaragoza.

Mpango wa Barcelona ni kuanzisha kizazi kipya na baada ya kumpata Lamine Yamal inapambana kumsajili Nico kwa sababu ameonyesha kucheza vizuri na Yamal wakiwa timu ya taifa ya Hispania huku pia kiwa ni mshkaji wa hadi nje ya uwanja wa kinda huyo mwenye kipaji aliyefunika katika fainali za Euro 2024.

Macho ya mabosi wa timu nyingi kubwa yanamtazama staa huyu ingawa ni Barcelona pekee ndio imeripotiwa kuanzisha mazungumzo rasmi na Bilbao.

Ripoti zinadai kwamba Nico anataka kwenda Barcelona ili kuwa karibu na mshikaji wake, Yamal, ambaye ndiye alimpa asisti ya bao la kuongoza la Hispania katika fainali ya Euro dhidi ya England.

WINGA wa Leeds, Crysencio Summerville, 22, amefanya mazungumzo na Chelsea ambayo inamhitaji kwa ajili ya kuboresha kikosi chao kwa msimu ujao wakati huo huo Rennes nayo imewasiliana na wawakilishi wake kuulizia huduma yake.

Staa huyu wa kimataifa wa Uholanzi alifanya vizuri msimu uliopita akiwa na Leeds ambapo alicheza mechi 49 za michuano yote na kufunga mabao 21.

WEST Ham imefikia katika hatua nzuri kwenye mazungumzo yao na Manchester United juu ya kumsajili beki wa kulia wa timu hiyo, Aaron Wan-Bissaka, 26, katika dirisha hili.

Bissaka ni mmoja kati ya wachezaji wanaodaiwa kuwekwa sokoni na Man United kwa ajili ya kupata pesa itakazotumia kufanya usajili mwingine utakaowaweka katika nafasi nzuri zaidi. Mkataba wa beki huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

BEKI wa zamani wa Liverpool, Joel Matip, ambaye ameachwa katika kikosi cha majogoo hao baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwisho wa msimu uliopita, yupo katika mazungumzo na kujiunga na Bayer Leverkusen katika dirisha hili. Matip ambaye ni mchezaji huru kwa sasa amependekezwa na kocha Xabi Alonso kwa ajili ya kufanya maboresho ya kikosi chake kwenye eneo la ulinzi.

AS Roma ni kati ya timu zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Lille, Jonathan David ambaye hadi kufikia sasa timu kibao zinatajwa kutaka kumsajili.

Jonathan ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Lille na msimu uliopita alicheza mechi 47 za michuano yote na kufunga mabao 26.

MSHAMBULIAJi wa RB Leipzig, Dani Olmo hana uhakika kama ataendelea kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao ama ataondoka wakati timu kibao zikihusishwa naye.

Olmo ambaye mkataba wake unamalizika 2027, yupo katika rada za Manchester City, Barcelona na Bayern Munich ambazo zimeonyesha kuvutiwa zaidi na kiwango alichoonyesha katika michuano ya Euro.

MCHEZAJI wa zamani wa Manchester City, Liverpool na timu ya taifa ya Italia, Mario Balotelli, 33, yupo katika hatua nzuri kwenye mazungumzo yake na Corinthians ya Brazil ili kujiunga nayo katika dirisha hili kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Adana Demirspor ya Uturuki. Balotelli msimu uliopita alicheza mechi 16 za michuano yote.

TOTTENHAM na Chelsea ni miongoni mwa timu zilizo katika vita ya kuiwania saini ya kiungo wa Rennes, Desire Doue, 19, kwa ajili ya kumsajili katika dirisha hili.

Staa huyu ambaye pia anawindwa na Bayern Munich na Paris Saint-Germain ambazo zimemwekea ofa nono mezani bado hajafanya uamuzi wa wapi atatua.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports, Rennes ipo tayari kumuuza staa huyu lakini inasubiria uamuzi wake juu ya wapi anataka kujiunga. Mkataba wa Doue unamalizika mwaka 2026.

Chanzo: Mwanaspoti