Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona yapanga kumtoa kafara Raphinha kisa Diaz

Frame 3 1 Barcelona yapanga kumtoa kafara Raphinha kisa Diaz

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona ameripotiwa kutaka kumpeleka Raphinha Liverpool ili kuipata saini ya Luis Diaz kwenye dirisha hili.

Inaelezwa moja kati ya maeneo ambayo Barca imeyapa kipaumbele katika dirisha hili ni la winga wa kushoto ambako anacheza Raphinha.

Licha ya kufunga mabao 10 kwenye mechi 37 za michuao yote, benchi la ufundi la wababe hao wa Nou Camp haliamini kwamba Raphinha anafaa kwenye eneo hilo kwani asili yake ni winga wa kulia, amekuwa akicheza hapo kwa kuwa hakuna mbadala.

Kwa sababu hiyo, Luis Diaz anaonekana kuwa mtu sahihi kutokana na kiwango alichoonyesha msimu uliomalizika, pia kiasili yeye ni winga wa kushoto.

Diaz ambaye mara kadhaa baba yake amekuwa akiweka wazi mtoto wake ana ndoto ya kucheza kwenye moja kati ya timu kubwa Hispania, kwa sasa hatma yake bado haijajulikana baada ya kuondoka kwa Jurgen Klopp hali inayowapa nguvu Barca wakiamini anaweza kukubali kujiunga nao.

Barca imekuwa ikihusishwa kutaka kumuuza Raphinha tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana lakini staa huyo amekuwa akigoma kuondoka na kusisitiza kwamba bado anataka kupambania namba kwenye kikosi cha kwanza.

Chanzo: Mwanaspoti