Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona yalazimishwa Sare na Napoli Camp Nou

Barca Vs Napoli Wachezaji wa Barca wakishangilia Goli la Penati la Ferran Torres

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ferran Torres amefunga goli la penati na kuipatia Barcelona alama moja kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Napoli katika sare ya 1-1 mtanange wa Ligi ya Europa uliopigwa Alhamis dimba la Camp Nou hatua ya 32.

Wakicheza kwa mara ya kwanza michuano hiyo baada ya angalau miaka 18, wababe hao wa soka la Hispania walijikuta wako nyuma kupitia bao la Piotr Zielinski wa Napoli.

Wakati upande wa Barcelona goli lao lilitokea kupitia matumizi ya video saidizi kwa refarii ambapo ilimuonyesha mlinzi Juan Jesus akiunawa mpira wa krosi ya Adama Traore.

Baada ya VAR hatimaye penati ikaamuriwa kupigwa, Torres akakwamisha mpira huo kwa kumpoteza kipa Alex Meret.

Kwa matokeo hayo, Barcelona watahitaji kushinda mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa Italia Februari 24, 2022 ili kufuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Europa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live