Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona yajitosa vitani saini ya Jadon Sancho

Sanchozzz (15).jpeg Barcelona yajitosa vitani saini ya Jadon Sancho

Thu, 27 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda wowote, Barcelona huenda wakatuma ofa kwenda Manchester United kwa ajili ya kutaka kumsajili winga wa mashateni wekundu hao, Jadon Sancho ambaye msimu uliomalizika alitolewa kwa mkopo kwenda Borussia Dortmund.

Sancho ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2026, hana mpango wa kurudi tena Man United ambako ameambiwa amuombe msamaha kwanza Erik ten Hag ili aruhusiwe kurudi katika timu hiyo.

Timu nyingi zimeonyesha nia ya kutaka kuipata huduma ya Sancho aidha kwa mkopo au kumnunua jumla na mbali ya Barca, Juventus na Dortmund zimeonyesha nia ya kumsajili.

Fundi huyu mwenye umri wa miaka 24, akiwa kwa mkopo Dortmund msimu uliopita alicheza mechi 21 za michuano yote na kufunga mabao matatu, akiiwezesha timu hiyo kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na ilipoteza mbele ya Real Madrid.

Kuna mechi ambazo alicheza kwa kiwango cha juu ikiwamo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Paris Saint-Germain ambayo aliweka rekodi ya kupiga chenga mara nyingi zaidi kwa msimu huu (12).

TOTTENHAM inataka kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace, Eberechi Eze, 25, katika dirisha hili na ipo tayari kutoa Pauni 60 milioni kwa ajili ya kuvunja mkataba wake. Kiasi hicho cha pesa kimewekwa katika mkataba wa Eze kwa timu itakayohitaji kumsajili.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 32 za michuano yote na kufunga mabao 11.

BRIGHTON ipo katika hatua nzuri katika mpango wake wa kutaka kumsajili kiungo wa Leicester City, Kiernan Dewsbury-Hall katika dirisha hili la uhamisho.

Hall ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, hata yeye ameonyesha nia ya kutaka kuondoka na kutua Brighton baada ya kuvutiwa na mipango ya timu hiyo inayotandaza boli.

MABOSI wa Bayern Munich bado wanahitaji kuipata saini ya kiungo Fulham, Joao Palhinha katika dirisha hili lakini changamoto kubwa inayokwamisha dili hilo lisikamilike hadi sasa ni wao kushindwa kufikia mwafaka wa masuala ya bei ya kiungo huyo.

Fulham inahitaji Pauni 60 milioni ili kumuuza Palhinha mwenye umri wa miaka 28, wakati ikiwa haipo tayari kutoa pesa hiyo.

ASTON Villa inataka kutuma wawakilishi wake kwenda Ureno kwa ajili ya kufanya mazungumzo ili kuipata saini ya winga wa Sporting Lisbon, Pedro Goncalves, 25, katika dirisha hili.

Pedro ambaye msimu uliopita alicheza mechi 49 za michuano yote na kufunga mabao 18, anaripotiwa anaweza kupatikana kwa zaidi ya Pauni 50 milioni. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2027.

IPSWICH imefikia patamu katika mazungumzo ya kumsajili beki wa West Ham, Ben Johnson ambaye mkataba wake unamalizika wiki ijayo. Staa huyu mwenye uraia wa England mwenye umri wa miaka 24, anataka kujiunga na Ipswich kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha West Ham. Msimu uliopita alicheza mechi 25 za michuano yote. Msimu uliomalizika akiwa na Hoffenheim kwa mkopo, alifunga mabao manane, katika mechi 31 za michuano yote. Dili hilo linaweza kukamilika baada ya fundi huyu kutoka katika michuano ya Euro.

MANCHESTER United ipo katika vita kali dhidi ya Arsenal na Aston Villa ili kuipata saini ya kiungo wa Juventus, Adrien Rabiot, ambaye tayari imeshaanza mazungumzo na wawakilishi wake sambamba na wale wa Juventus. Rabiot ambaye kwa sasa anaitumikia Ufaransa katika michuano ya Euro inayoendelea kule Ujerumani, mkataba wake unamalizika mwisho wa wiki hii.

KIUNGO wa Leeds United, Marc Roca, 27, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Real Betis, yupo katika mazungumzo ya kusaini mkataba wa kudumu wa kuendelea kusalia katika timu hiyo.

Roca hahitaji kurudi tena Leeds kwa sababu anataka kucheza Ligi Kuu na timu hiyo itashiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live