Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona yageuka kwa Kingsley Coman

Kingsley Coman.png Barcelona yageuka kwa Kingsley Coman

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya imeelekeza nia yake ya usajili kwa winga wa Bayern Munich, Kingsley Coman baada ya kushindwa majaribio kupata saini ya Nico Williams kutoka Athletic Club. (El Nacional - Spain)

Napoli imefungua mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa Scotland, Scott McTominay, 27, na ingependelea dili la mkopo. (Times - subscription required)

Pia Napoli inakaribia kumsajili kiungo wa Scotland, Billy Gilmour, 23, kutoka klabu ya Brighton & Hove Albion. (Corriere dello Sport - in Italian)

Chelsea imerejea katika mazungumzo na Napoli kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen,25. (Talksport)

Paris Saint-Germain imeanza kupunguza nia yake ya kumsajili winga wa Manchester United, Jadon Sancho,24, na sasa inafikiria kujiondoa katika mbio za kumsajili Osimhen.

West Ham United inapanga dili kumsajili Tammy Abraham,26, wa timu ya Roma huku klabu hiyo ya Serie A ikikusudia kumuuza mshambuliaji huyo kwa pauni milioni 25. (Gazzetta dello Sport via Football Italia)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live