Barcelona inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuipata saini ya straika wa Chelsea na Ujerumani, Timo Werner, 25, kwa mkopo katika dirisha lijalo la majira ya baridi.
Werner anaonekana kama mbadala wa Raheem Sterling ambaye Barca ilihitaji kuipata huduma yake katika dirisha la majira ya baridi lakini mabosi wa Man City wanataka kusalia naye hadi mwisho wa msimu.
Werner mwenyewe anatamani sana kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea na tangu msimu huu uanze mechi alizoanza kwenye kikosi cha kwanza ni nne na zilizobakia nyingi alikuwa akiingia akitokea benchi.
Man City imegoma kumuachia Sterling staa huyo katika dirisha lijalo kwa sababu haina uhakika wa kuipata huduma ya straika wa Tottenham, Harry Kane.
Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2025. Msimu huu amecheza mechi 10 za michuano yote na kufunga mabao mawili.