Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona wamtaja Mohammed Kudus

Mohammed Kudus Mohammed Kudus

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Barcelona inayocheza ligi kuu ya nchini Hispania imeripotiwa kuvutiwa na mchezaji wa taifa la Ghana Mohamed Kudus (22), ambaye amekuwa na kiwango kizuri sana tangua kuanza kwa michuano hii ya kombe la dunia nchini Qatar.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa Barcelona Jordi Cruyff ambaye ni Mkurugenzi wa Michezo, inaeleza kuwa wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu sana Mohamed Kudus huku akiweka wazi kuwa anaivutia sana klabu hiyo.

“Tumekuwa tukimfuatilia Mohamed Kudus kwa zaidi ya mwaka, hatuweza kusema kwamba Barca wanamtaka Kudus lakini anavutia. Anafunga mabao na Holland wanazungumzia zaidi kuhusu nafasi yake, hivyo namjua mno yeye” Alisema Cruyff.

Mohamed Kudus anaichezea klabu ya Ajax kwenye nafasi ya kiungo wa kati, na amekuwa na mchango mkubwa pia hata kwenye timu yake ya taifa ya Ghana akiwa ameifungia mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Korea ambao walishinda kwa jumala ya 3-2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live