Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona na rekodi mbovu UEFA

Fbl Eur C1 Barcelona Bayern 1 1 1000x600 Barcelona na rekodi mbovu UEFA

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Barcelona imeweka rekodi mbovu katika historia ya klabu yao baada ya kuondoshwa mapema katika michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya kwenye hatua ya makundi mara mbili mfululizo kabla ya mechi yao ya sita, ilipomenyana dhidi ya Bayern Munich uliyochezwa usiku wa kumkia leo.

Mara ya mwisho Barcelona kung'oka katika michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya mara mbili mfulilizo ilikuwa msimu wa 1998-99 kabla ya kuvunja rekodi hiyo mbovu usiku wa kuamkia jana.

Barcelona ilipokea kichapo cha mabao 3-0 katika uwanja wao wa nyumbani Nou Camp, na vijana wa Xavi Hernandez wameungana na Arsenal, Manchester United, Juventus katika michuano ya Europa ambayo safari hii vigogo hao watachuana vikali.

Baada ya kipigo hicho Barcelona imejikita nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne baada ya kufungwa michezo mitatu na kushinda mechi moja ilipomenyana na Viktoria Plzen ambayo usiku wa kuamkia jana iipokea kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Inter Milan.

Inter Milan ilifanikiwa kuipiku Barcelona licha ya kusuasua mechi za mwanzo kwa tofauti ya pointi sita na kufuzu raundi ya 16 bora ya michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu huu.

Licha ya kukumbwa na janga la uchumi Barcelona ilitumia kitita cha Pauni 150 milioni kwaajili ya usajili hata hivyo mastaa hao wameshindwa kuivusha timu hiyo raundi inayoufuata ya mtoano.

Barcelona ilitumia mkwanja huo kwa kuwasajili Robert Lewandowski, Jules Kounde, Raphinha, Franck Kessie, Andreas Christensen, Marco Alonso, na Hector Bellerin aliyejiunga bure.

Awali Barcelona ilikuwa na malengo ya kutinga robo fainali ya michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu huu lakini sasa imeangukia pua.

Kabla ya kipigo cha Viktoria Plzen walichopata dhidi ya Inter Milan, Xavi alikuwanna matumaini timu hiyo ingetubia mpango hata hivyo matokeo hayakuwa hivyo.

"Tutaangalia marejeo ya timu nyingine kabla ya mechi, tunatakiwa kuonyesha kwamba tunaweza kucheza dhidi ya timu hizi bila kuwa na hofu," alisema Xavi kabla ya mechi hizo.

Chanzo: Mwanaspoti