Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona na mahesabu ya Haaland, anatakiwa Catalunya

Halaand Erling Braut Haaland

Tue, 14 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Barcelona Joan Laporta amesema kwamba anaangalia namna ya kutafuta njia ya kuipata saini ya mashambuliaji wa Dortmund Erling Haaland.

Licha ya changamoto za kifedha katika klabu ya Barcelona lakini wapo tayari kumwaga pesa ya kutosha kwa fowadi huyo wa kimataifa wa Norway kwani iko wazi kwamba Barcelona wana tatizo katika eneo la ushambuliaji kwa kushindwa kupata idadi kubwa ya mabao kwenye mechi zao.

Kwa ubora wake katika eneo la kushambulia, umri wake na wasifu wake, Barcelona wanamuona Haaland kama chaguo bora, mchezaji ambaye wanaweza kuona faida kubwa, ndani na nje ya uwanja. Sehemu ngumu, bila shaka, itakuwa kukamilisha dili hiyo.

Kuna uvumi mkubwa unaoendelea kwamba Haaland anaweza kupatikana mwisho wa msimu lakini dau bado inasemekana kuwa linacheza kwenye euro milioni 70. Halafu, kuna mshahara wa mchezaji na ada ambayo wakala wake, Mino Raiola ataafiki.

Laporta hajaonyesha dalili zozote za kukata tamaa na ataendelea kuwinda saini ya mchezaji huyo nyota wa Bundesliga mpaka mwisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live