Kuna kitu kinaitwa MOVEMBA, ikiwa ni muunganiko wa maneno mawili; Moustache (Mo) na Novemba (Vemba).
Kwa kifupi MOVEMBA ni Novemba ya Mustachi.
Hili ni tukio maalumu ambalo hufanyika mwezi Novemba likihusisha wanaume kufuga mustachi kama ishara ya kukuza uelewa kuhusu changamoto za kiafya kwa wanaume.
Changamoto hizo ni kama tezi dume, saratani ya korodani, na mambo mengine kama kujinyonga nk.
Movemba ni harakati za taasisi inayoitwa Movember Foundation, ambayo huchangisha fedha na kutoa elimu kwa wanaume kufanya vipimo mara kwa mara na kupata matibabu sahihi na ya wakati ili kupunguza madhara ya magonjwa hayo.
Kupitia kampeni hii, wanaume wanaofuga mustachi kwa ajili ya Movemba huitwa Mo Bros, na wanawake wanaounga mkono harakati hizi huitwa Mo Sisters.
Wachezaji wa Barcelona nao wamefuga mustachi kama kuunga mkono harakati hizi.