Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona kuzoa viungo watatu EPL

Xavi Hernandez Coach Kocha wa FC Barcelona, Xavi Hernandez

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Barcelona inaelezwa wanavizia saini za wachezaji watatu kutoka ligi kuu ya England katika dirisha dogo la mwezi Januari mapema baada ya kupita michuano ya kombe la dunia.

Miamba hiyo ya soka nchini Hispania imepanga kuboresha eneo la kiungo la klabu hiyo ndo maana anatafuta saini za viungo watatu kutoka ligi kuu ya Uingereza wakiongozwa na kiungo wa klabu ya Chelsea Jorginho raia wa Italia.

Barcelona ambao wanashika nafasi ya pili kunako ligi kuu ya Hispania huku wakiwa kwenye hatihati ya kutofuzu hatua ya 16 bora kwenye ligi ya mabingwa ulaya huku timu hiyo ikonekana bado haijakaa sawa chini ya kocha Xavi.

Viungo wengine ambao Barcelona inawatolea macho ni Youri Tielemans kutoka Leicester na Ruben Neves kutoka Wolverhampton Barca wanahitaji wachezaji hawa ili kuimarisha timu hiyo na kuirudisha kwenye ubora wake.

Miamba hiyo ya Catalans kupitia rais wake Laporta ambae alisema wataingia sokoni Januari kuboresha kikosi chao hivo tutarajie lolote kutoka kwenye klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live