Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona kuwasajili jumla Cancelo, Felix

Cancelo X Felix Barcelona kuwasajili jumla Cancelo, Felix

Sat, 23 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Barcelona ipo kwenye mpango wa kufanya uhamisho wa jumla wa Joao Felix na Joao Cancello raia wa Ureno waliopo kikosini hapo kwa mkopo kutokea Atletico Madrid na Manchester City.

Tayari klabu ya Barcelona imeshafahamu kiasi kitakachotumika kukamilisha usajili huo, Barca itabidi wailipe Manchester City € 25 Million ili wainase saini ya Cancello ambaye hayupo kwenye mipango ya Pep Guardola.

Kwa upande wa Joao Felix wanapaswa kuilipa Atletico Madrid € 80 Million, lakini ili haya yote yafanikiwe Barcelona wanapaswa kuwauza baadhi ya nyota wake kutokana na sakata linalowakabili la matumizi makubwa ya pesa.

Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amesema kwasasa wataangalia uwezekano wa kumsajili Cancello ambaye ana bei rahisi na baadae watamsajili Felix.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live