Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona kumshtaki Rais wa La Liga

Joan Laporta JOAN Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupitia kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii, Barcelona wametoa taarifa wakisema wamekerwa sana na habari iloyotolewa na La Vanguardia asubuhi ya juzi na wangependa kumuona rais huyo wa Laliga akitoa maelezo haraka.

Taarifa hiyo inasema: "FC Barcelona inaelezea hasira, hasira nyingi kuhusiana na taarifa iliyotolewa na La Vanguardia kuhusu Javier Tebas. Rais wa La Liga anapaswa kujitokeza hadharani kutoa maelezo na Kujiuzulu kutoka kwa nafasi yake."

Joan Laporta na bodi wanasema: "Si mara ya kwanza Tebas kutumia vyombo vyake vya habari kuiharibu Barcelona lakini, mbali na matendo yake ya kawaida, hatukuwahi kufikiria kwamba angejaribu kuharibu klabu yetu kwa ushahidi wa uongo."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live