Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona kumpiga "kitanzi" Ronald Araujo

Barcelona Centre Back Ronald Araujo Ronald Araujo

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Barcelona wako kwenye mchakato wa kumuongezea mkataba beki wake raia wa kimataifa wa Uruguay Ronald Araujo akiwa amepewa kipaumbele kikubwa zaidi.

Beki Ronald Araujo amekua moja ya wachezaji muhimu zaidi ndani ya klabu ya Barcelona hivi karibuni na ndio sababu kubwa ya klabu hiyo kutoka kumuongezea mkataba mrefu zaidi.

Mkataba wasasa wa beki huyo wa kimataifa wa Uruguay unamalizika mwaka 2026, Lakini mabingwa hao wa soka kutoka nchini Hispania wanahitaji kumpa mkataba mrefu zaidi beki huyo.

Ronald Araujo ameonesha kiwango bora sana ndani ya klabu hiyo katika misimu mitatu ya hivi karibuni, Jambo ambalo limemfanya beki huyo kua moja ya manahodha wa klabu hiyo.

Klabu ya Barcelona wanahitaji kutengeneza kizazi kipya ambacho kitakuja kufanya makubwa katika siku za usoni ndani ya klabu hiyo, Na ndio sababu kubwa ya kuwaongezea mikataba wachezaji wake muhimu na wenye umri mdogo kama beki Ronald Araujo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live