Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona kumpa mkataba mpya Gavi

Gavi Bareclona Gavi

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Barcelona wanajiandaa kumpa mkataba mpya kinda wao Gavi wa miaka mitano na kuwa miongoni mwa wachezaji makinda waliopewa mikataba mirefu baada ya Pedri na Ansu Fati.

Gavi ambaye anacheza nafasi ya kiungo amefikisha miaka 17 mwezi agosti na amefanikiwa kuingia kwenye timu ya wakubwa msimu huu na ameshacheza michezo 14 kwenye mashindano yote msimu huu kwenye kikosi cha Barcelona.

Gavi amefanikiwa kuingia kwenye timu ya taifa ya Hispania, na anatarajiwa kuwepo kwenye kikosi kitakacho cheza michezo ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Ugiriki na Swideni.

Umekuwa mwanzo mzuri kwa kijana Gavi ambaye bado yuko kwenye mazungumzo na klabu ya Barcelona ambayo ipo tayari kumpa mkataba wa muda mrefu na nyongeza ya mshahara kwa kila msimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live