Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona kumgeukia De Gea

Manchester United Wambembeleza De Gea Kurejea Old Trafford David De Gea

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Barcelona imeripotiwa kuwa na mpango wa kumpata kipa wa zamani wa Manchester United, David de Gea.

Kipa huyo Mhispaniola mwenye umri wa miaka 33, amekuwa hana timu tangu alipoachana na Man United mwishoni mwa msimu uliopita.

Hakuwa na uchache wa ofa, ambapo klabu kibao zimekuwa zikihitaji huduma yake zikiwamo za England na Saudi Arabia. Lakini, taarifa za hivi karibuni ni kwamba De Gea mwenyewe anapendelea kubaki Hispania wakati atakapofanya uchaguzi wa klabu yake ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa za kutoka Hispania, anaweza kuwa na nafasi ya kujiunga na Barcelona na kinachosemwa mkali huyo anawindwa na miamba hiyo ya Nou Camp.

Kutokana na timu kukabiliwa na matatizo ya kifedha, uamuzi wa kumchukua kipa huyo wa bure, bila shaka utapewa nafasi kubwa na wababe hao wa Nou Camp. Hiyo ina maana, De Gea atakwenda kuwa kipa namba mbili nyuma ya Marc-Andre ter Stegen, ambaye anahusishwa na mpango wa kwenda Saudi Arabia.

Kipa huyo Mjerumani, Ter Stegen amekosa mechi 17 kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mgongo na hivyo kipa wa kutokea kwenye akademia ya La Masia, Inaki Pena, ndiye anayedaka kwa sasa.

Lakini, kinda huyo wa kimataifa wa Hispania wa timu ya vijana chini ya miaka 21 hana ubora mkubwa sana na uzoefu wa kutosha wa kuhimili mikikimikiki ya kibabe. De Gea aliondoka Man United mwaka jana akiwa ametumikia timu hiyo kwa miaka 12 na kucheza mechi 545. Msimu wake wa mwisho Man United alichaguliwa kuwa Kipa Bora wa Ligi Kuu England.

Chanzo: Mwanaspoti