Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona hoi La Liga, Koeman hana presha

Skysports Barcelona De Jong 5522406 Wachezaji wa Barcelona wakimzonga mwamuzi baada ya kumuonyesha kadi nyekundu Frank de Jong

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wababe wa Catalunya, klabu ya Barcelona mambo yanazidi kuwaendea ndivyo sivyo baada ya usiku wa jana kulazimishwa sare na timu ya Cadiz.

Huu ni mchezo wa pili mfululizo kwa Barca kusuluhu ndani ya La liga baada ya siku nne zilizopita kulazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Granada katika dimba la Camp Nou.

Katika mchezo wa jana Barca wameshuhudia wakimaliza mchezo huku wakiwa pungufu mara baada ya Kiungo wake Mdachi, Frank De Jong kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 65 ya mchezo.

Matokeo wanayopata Barcelona yanazidi kuongeza presha kwenye benchi la ufundi la timu hiyo lakini Kocha Ronald Koeman, amesema yeye hasikilizi kelele za nje ya uwanja bali anachozingatia ni kuona namna gani timu inaimarika pale ambapo ina mapungufu.

Rais wa Barcelona Joan Laporta na mashabiki wa timu hiyo wameonesha wazi wazi kutofurahishwa na uwepo wa kocha huyo kama mwalimu wa Barcelona.

Barcelona inashika nafasi ya saba La Liga wakiwa na pointi zao 9 baada ya kushuka dimbani mechi tano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live