Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona haiwapi heshima nyota wake wa zamani

Xavi Kusalia Kama Kocha Wa Barcelona Hadi Juni 2025 Aliyekuwa Kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa klabu ya Sevilla Quique Sanchez ameeleza kuwa klabu ya Barcelona haiwatendei haki nyota wazamani waliovujà jasho na damu kwa ajili ya kuipambania klabu hiyo.

Sanchez amebainisha kuwa klabu hiyo haiwatendei haki nyota hao ikiwemo Xavi Hernandez, Koeman na Leonel Messi.

"Napaswa kusema haya, lakini sijui kwanini Barcelona hawawapi heshima inayotakiwa wachezaji wao wa zamani."

"Ni kitu kibaya sana, walianza na Koeman, kwa Messi, na sasa Xavi.Ni mbaya sana, natamani klabu ingewapa heshima inayostahili wachezaji wao wa zamani, hiyo ingekua nzuri."

"Xavi ni kocha aliyejitoa kwa mengi kwa ajili ya klabu, amekumbana na mambo mengi kama mchezaji na amefanya kazi nzuri kama kocha.

Huo ndio uungwana wa kuwa karibu.Hiki kinaunganisha sana, kuwapa heshima nyota wa zamani ni kitu muhimu sana."

- Kocha wa Sevilla Quique Sanchez akieleza kile ambacho kilichowatokea nyota wa zamani wa Barcelona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live