Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona gari limewaka, watoa kichapo kwa Madrid

Barcelona 6.png Wachezaji wa Barca, wakimpongeza Aubameyang ambae alitupia magoli mawili

Mon, 21 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana wa Xavi Hernandez, Timu ya Barcelona imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Real Madrid katika mchezo wa La Liga (El Classico) Jumapili Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.

Mabao ya Barcelona yamefungwa na Pierre-Emerick Aubameyang mawili, dakika ya 29 na 51, Ronald Araujo dakika ya 38 na Ferran Torres dakika ya 57.

Kwa ushindi huo, Barcelona inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 28 na kusogea nafasi ya tatu, sasa ikizidiwa pointi 12 na Real ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.

Huenda huu ukawa ni mwanzo wa zama mpya baada ya Timu hiyo ya Catalunya kufanya vibaya katika kipindi cha miezi sita iliyopita kabla ya ujio wa Mkongwe Huyo aliepita Barca na kufanya makubwa.

Barca wamekuwa na muendelezo mzuri katika mechi za hivi karibuni kuanzia meichezo ya Uropa mpaka La Liga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live