Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona Vs Frankfurt, rekodi zao ni kiboko

Barcelona.jpeg Mchezo wa mkondo wa kwanza Barcelona na Frankfurt zilitoka sare ya bao 1-1

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: eatv.tv

Wachezaji Memphis Depay, Sergino Dest na Gerard Pique wamejumuishwa kwenye kikosi cha FC Barcelona kitakachocheza mchezo wa robo fainali ya Europa League dhidi ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani baada ya kupona majeruhi. Leo Usiku katika Dimba la Camp Nou.

Kurejea kwa wachezaji hawa kunampa upana zaidi wa kikosi kocha Xavi Hernandez kuchagua wachezaji wataoanza kwenye mchezo wa usiku wa leo ambao ni wa mkondo wa pili wa hatua ya robo fainali. Mchezo wa mkondo wa kwanza timu hizi zilitoka sare ya bao 1-1, mchezo uliochezwa nchini Ujerumani wiki iliyopita.

Licha ya Memphis Depay, Sergino Dest na Gerard Pique kurejea lakini bado kocha xavi atakosa huduma za wachezaji kama Dani Alves ambaye atakosekana kwa sababu za kikanuni, lakini Samuel Umtiti, Sergi Roberto na Ansu Fati wote wanamajeruhi. Lakini pia Pique amejumuhishwa kwenye kikosi lakini hayupo fiti kwa asilimia 100 kuanza kwenye mchezo huu.

Timu zote mbili zinarekodi bora kuelekea mchezo huu, FC Barcelona imepoteza michezo 2 tu kati ya 16 dhidi ya timu kutoka nchini Ujerumani, wakati Frankfurt haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye michezo 9 ya mwisho waliocheza dhidi ya timu kutoka Hispania wameshinda michezo 5 na sare 4, na katika michezo 4 ya mwisho wameshida 3 na sare 1.

Baada ya sare ya mchezo wa kwanza na  kufutwa kwa kanuni ya goli la ugenini timu itakayoshinda mchezo wa leo usiku itafuzu hatua ya nusu ifainali.

Chanzo: eatv.tv