Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona: Ruksa Kumchezesha Ferran Torres

GettyImages 1362518769 1 Ferran Torres

Mon, 10 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Barcelona imethibitisha kuweza kumsajiri rasmi mchezaji waliyemnunua kutokea klabu ya Manchester City Ferran Torres, baada ya kukubaliana mkataba mpya na mlinzi wake mahiri Samuel Umtiti ambaye amekubali kupunguza mshahara wake.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania amejiunga na klabu ya Barc akitokea klabu ya Manchester City kwa mkataba wa miaka mitano na nusu, huku mkataba wake ukiwa na thamani ya Pauni milioni 46.7.

Klabu ya Barcelona miezi ya karibuni walikuwa na kipindi kigumu cha ukata wa fedha, lakini waliweza kumsajiri Torres baada kufanikiwa kupata mkopo kutoka bank ili kuweza kuendesha klabu.

Leo Jumatatu, shirikisho la mpira wamiguu nchini Hispania La Liga wametangaza kuwa kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati mlinzi wakimataifa kutoka ufaransa Umtiti, kukubali kupunguza mshara wake klabu ya Barcelona wamefanikiwa kumsajiri Torres kwenye timu ya wakubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live