Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona, Arsenal vitani leo Ligi ya Mabingwa

Barcelona, Arsenal Vitani Leo Ligi Ya Mabingwa Barcelona, Arsenal vitani leo Ligi ya Mabingwa

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Barcelona na Arsenal, leo zitatakiwa kufanya kazi kubwa ili kuhakikisha zinatinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Arsenal ambayo ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Porto kwenye mchezo wa kwanza ugenini, leo itakuwa nyumbani kuhakikisha inapindua matokeo hayo ili iweze kufuzu kwenye hatua hiyo muhimu.

Kwa upande wa Barcelona ambayo ilionyesha kiwango cha juu kwenye mchezo wa kwanza ugenini na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Napoli, leo inarejea nyumbani kuhakikisha inapata ushindi na kufuzu.

Mabingwa watetezi wa michuano hiyo mikubwa Ulaya Manchester City pamoja na mabingwa wa kihistoria Real Madrid tayari zimeshafuzu sawa na Bayern Munich na Paris Saint-Germain.

Timu zote zinazocheza leo na kesho zina nafasi ya kufuzu kutokana na matokeo ya michezo ya mkondo wa kwanza kwa kuwa hakuna iliyopoteza kwa zaidi ya bao moja.

Matokeo mechi tano za nyuma Arsenal vs Porto: Arsenal 4-0 Porto Porto 2-0 Arsenal Porto 2-1 Arsenal Arsenal 4-0 Porto Porto 1-0 Arsenal.

Mechi tano za Barcelona vs Napoli Napoli 1 – 1 FC Barcelona Napoli 2 – 4 FC Barcelona FC Barcelona 1 - 1Napoli FC Barcelona 3 – 1 Napoli Napoli 1 – 1 FC Barcelona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live