Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barca yazidi kupeta La Liga

Fbl Liga Esp Elche Barcelona Scaled Wachezaji wa Barcelona wakishangilia goli la kusawazisha

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wawili wa kutokea bechi Ferran Torres na Memphis Depay wamefunga mabao na kuipa Barcelona alama tatu muhimu mbele ya timu iliyoonyesha ushindani wa hali ya juu ya Elche mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga uliomalizika 2-1.

Elche ambao wako nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi hiyo walipata bao la kuongoza kupitia kwa nahodha Fidel aliyetumia makosa ya kiungo Pedri.

Hata hivyo, kipindi cha pili kocha Xavi alifanya mabadiliko ambayo yalitosha kuwapa nguvu hasa kwa Torres ambaye aliongeza kasi ya mchezo na kupelekea goli lake na la ushindi kwa mkwaju wa penati iliyofungwa na Depay.

Ushindi wa Barca unaifanya kupanda mpaka nafasi ya tatu ingawa wanaweza kukaa kwa muda endapo Real Betis watashinda kwa Atletico Madrid.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live