Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barca yatosa ofa nono ya kinda Yamal

Lamine Yamali Tuzo Barca yatosa ofa nono ya kinda Yamal

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Barcelona imeendelea kukataa ofa kwa ajili ya kinda wake, Lamine Yamal, ikisisitiza winga huyo hauzwi.

Yamal ametoboa na kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona mwaka jana alipokuwa na umri wa miaka 15 tu na tangu wakati huo amekuwa moto, wakati aliweka rekodi ya kuwa kinda wa tano kwenye historia ya La Liga, na ndani ya muda huo hadi sasa, tayari anaichezea timu ya taifa ya Hispania, ambapo yupo na chama hilo la La Roja huko kwenye fainali za Euro 2024.

Wakati akitazamwa kama mmoja wa mastaa wanaokuja kwa kasi kwenye dunia ya soka, Yamal amezivutia timu nyingi zinazohitaji saini yake ikiwamo PSG, ambayo imepanga kuvunja rekodi ya dunia kwenye usajili wake, hasa kwa kipindi hiki wana-chotafuta mrithi wa Kylian Mbappe.

Machi mwaka huu, rais wa Barcelona, Joan Laporta alisema klabu hiyo ilikataa ofa ya Pauni 169 milioni (Euro 200 milioni) ya kumuuza mchezaji Yamal kutoka kwa klabu ambayo hakuitaja, aliposema: “Tulipokea ofa kwa ajili ya wachezaji wetu kama Lamine Yamal, Euro 200 milioni na niliwaaambia hapana.

“Kwa sababu tunamwaamini kijana wetu, kwasababu ndiye hatima ya timu yetu. Tunaamini kwenye ubora wake, tupo katika kipindi cha kujitafuta kiuchumi, lakini hilo litafika mwisho.”

Lakini, ripoti zinadai kwamba PSG ipo tayari kuongeza dau la kumnasa Yamal na kufikia Pauni 211 milioni (Euro 250 milioni), ambayo itakuwa rekodi mpya kwenye uhamisho wa wachezaji, ikivunja ile ada ya Pauni 198 milioni (Euro 222 milioni), ambapo PSG yenyewe iliilipa Barcelona kunasa huduma ya supastaa wa Kibrazili, Neymar mwaka 2017.

Kwenye mkataba wa Yamal kuna kipengele kinachofichua kwamba kwa timu itakayohitaji kuvunja mkataba wa timu hiyo bila ya Barca kuridhia kumuuza, basi itahitaji kulipa Pauni 846 milioni (Euro 1 bilioni).

Deco pia alikaririwa akisema Yamal ana maafikiano ya kubaki Barca kwa miaka 8.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live