Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barca out UEFA, yavunja rekodi ya miaka 17

Barca Elinated Wachezaji wa Barcelona wakiwa wamenyong'onyea kwa kichapo

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa mara tano wa Ulaya FC Barcelona wametolewa rasmi kwenye mashindano hayo kufuatia kupata kipigo cha goli 3-0 kutoka kwa Bayern Munich mchezo uliopigwa dimba la Allianz Arena Jumatano Disemba 8.

Kipigo hicho kinaifanya Barca sasa kuangukia kwenye michuano ya Ligi ya Europa ambapo inakuwa mara ya kwanza katika miaka 17 iliyopita klabu hiyo kushindwa kufuzu kucheza hatua ya 16 bora, mara ya mwisho ikuwa ni msimu wa 2003/04

Kutolewa huko ni mwendelezo wa wakati mgumu ambao klabu hiyo imekuwa ikikutana nao hasa baada ya mdodoro wa uchumi ambao ulipelekea hata kuondoka kwa nyota Lionel Messi na kujiunga na Paris St-Germain.

Barca walikuwa wanahitaji ushindi ili wafuzu hata hivyo wameshindwa na kibaya zaidi Benfica wakashinda bao 2-0 dhidi ya Dynamo Kyiv ambapo wameiacha nafasi ya tatu ambapo watacheza mchezo wa mtoano kupata tiketi ya kucheza michuano ya Uefa ndogo.

Mabao ya Bayern Munich ambayo imeshinda mechi zote sita hatua ya makundi yamefungwa na Thomas Muller, Leroy Sane na Jamal Musiala ambaye alimalizia pasi ya Alphonso Davies.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live