Barcelona imeendelea kuchechemea katika kupata matokeo kwenye mechi za Ligi Kuu nchini Hispania La Liga hii ni baada ya kutoa sare ya goli 1-1 na timu yenye wachezaji 10 Sevilla.
Mtanange huo umepigwa Jumanne Disemba 21, ambapo matokeo hayo yanaifanya Sevilla kuendelea kushikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga alama tano pungufu ya kinara Real Madrid wakati sare imeipotezea nafasi ya kushika nafasi ya nne sasa inashika nafasi ya saba.
Sevilla walikuwa wa kwanza kufunga goli kupitia kwa Alejandro Gomez akimalizia pasi ya Ivan Rakitic ambapo Barcelona wakasawazisha goli hilo kupitia kwa Ronald Araujo.
Mlinzi Jules Kounde ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu mbalimbali Ulaya, alionyeshwa kadi nyekundu kufuatia kucheza madhambi kwa Jordi Alba.
Barca watasafiri kuwakabili Mallorca Januari 2.