Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barca, Girona kumpima presha carlo Ancelotti

Girona Warejea Kileleni Mwa LaLiga Baada Ya Kuwachapa Barcelona 4 2 Barca, Girona kumpima presha carlo Ancelotti

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Hadi kufikia asubuhi ya jana Ijumaa, msimamo wa La Liga ulivyokuwa ukisoma, Real Madrid ipo kileleni kwa tofauti ya pointi saba dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili, Girona.

Pointi nane dhidi ya Barcelona kwenye nafasi ya tatu. Lakini, miamba hiyo ya Nou Camp ilikuwa na nafasi ya kupunguza pengo hilo la pointi na kubaki tano endapo kama itakuwa imeibuka na ushindi dhidi ya Mallorca katika mchezo uliotarajia kufanyika uwanjani Nou Camp usiku wa jana Ijumaa. Ushindi wa Barca utawasaidia pia kuwashusha Girona kwenye nafasi ya pili na kuweka pengo la pointi mbili dhidi yao wakati mchakamchaka huo wa La Liga ukiingia kwenye wiki ya 28.

Girona yenyewe shughuli yake itakuwa leo, Jumamosi itakapokipiga na Osasuna katika moja ya mechi kali kabisa katika wikiendi hii. Kasi ya Girona uwanjani kwa sasa imeshuka, ambapo imeambulia vipigo vitatu katika mechi nne na hivyo kufifisha matumaini ya kubeba ubingwa.

Na kama wataendelea na kasi hiyo hafifu, basi wataondoshwa kwenye nafasi ya pili na pengine hali inaweza kuwa mbaya zaidi na kukosa nafasi kwenye Top Four ili kukamatia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Daley Blind huenda akarejea na kuanza kwenye kikosi cha Girona sambamba na David Lopez kwenye sehemu ya kiungo.

Osasuna inakosa huduma ya beki muhimu David Garcia, hivyo inaweza kucheza mfumo wa kutumia mabeki watatu na washambuliaji wawili, Raul Garcia na Ante Budimir baada ya kufanya kweli wikiendi iliyopita.

Ushindi kwa Girona utafanya pengo la pointi kubaki kuwa nne dhidi ya Real Madrid, ambayo yenyewe itasubiri hadi kesho Jumapili kukipiga na Celta Vigo huko Bernabeu.

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti anaamini kwenye uwezo wa kikosi chake na kwa kuwa mechi hiyo inachezwa nyumbani, uhakika kwao ni mkubwa kwamba watarudisha pengo la pointi na kuwa kama lilivyokuwa hata kama Girona na Barcelona zitakuwa zimeshinda mechi zao.

Valencia itakuwa na shughuli pevu hii leo mbele ya Getafe mchezo uliobeba hisia kubwa, ambapo wageni kwenye mchezo huo watakosa huduma ya mshambuliaji matata, Mason Greenwood anayetumikia adhabu.

Diego Simeone na chama lake la Atletico Madrid naye atakuwa mzigoni, akikipiga na Cadiz ugenini. Barca kama itakubali kuchapwa na Mallorca, basi ushindi wa Atletico Madrid utawapandisha hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa La Liga, kwa sababu itakuwa imefikisha pointi 58, lakini yenyewe ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Granada na Real Sociedad nao ni mshikemshike katika mechi yao matata kabisa itakayofanyika leo huko Estadio Nuevo Los Carmenes. Mechi hiyo inakutanisha timu zenye upinzani mkali, hasa baada ya matokeo yaliyopita, ambapo Sociedad iliibuka na ushindi wa mabao 5-3.

Mechi nyingine za kesho, La Palmas ilikuwa nyumbani kukipiga na Athletic Bilbao, wakati Real Betis itakuwa na kasheshe zito mbele ya Villarreal.

Jumatatu kutakuwa na mchezo mmoja tu, ambapo Almeria ilikuwa nyumbani kukipiga na Sevilla katika mechi zinazotarajiwa kuwa na mvuto mkubwa.

Chanzo: Mwanaspoti