Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barbara atoa kauli Simba SC

Simba Sc Ceo Gonzalez Barbara R924u3yxx0511g9tf2b3fbsh4 Barbara Gonzalez

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa Simba walishaingiwa ubaridi baada ya mitandao ya kijamii kuanika kuwa Mtendaji Mkuu wa Barbara Gonzalez ameachia ngazi, lakini mwenyewe amevunja ukimya na kusisitiza yupo sana Msimbazi licha ya changamoto anazopitia.

Usiku wa juzi kupitia kurasa za mitandao ya klabu hiyo iliweka taarifa kuna ujumbe utakazungumzwa na Barbara ila baada walieleza jambo hilo limeshindikana.

Barbara alisema alikuwa anataka kushukuru, kuzungumza na mashabiki wa Simba kuhusiana na mambo mengi muhimu yaliyotokea kwenye klabu msimu uliopita pamoja na mipango yao ya msimu ujao.

Jambo hilo lilishindikana kufanyika kutokana mambo ya ndani kwenye klabu yalikwenda tofauti kama vile alivyokuwa akitarajia hadi morali na hali yake ya kupambana kwa ajili ya timu ilishuka.

Barbara alisema hakuwa kwenye hali nzuri wakati aliyotakiwa kuzungumza masuala ya timu kutokana na mambo fulani ya ndani hayakwenda kama vile alivyokusudia lililomfanya morali yake kushuka.

“Niweke wazi kwa sasa siwezi kuondoka wala kufikiria kuacha kazi yangu hii bado nipo nipo naendelea na majukumu ya kazi kwani changamoto ni sehemu ya safari katika mafanikio,” alisema Barbara na kuongeza;

“Bado nipo Simba na naendelea kufanya majukumu yangu ya kila siku na niwambie Kwamba (juzi saa 5:30 asubuhi) nipo njiani kwenda Airport, nasafiri nje ya nchi, kwa shughuli muhimu ya klabu yetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live