Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barbara apewa kazi tatu ngumu Simba

Barbar Simba Pic Data Barbara apewa kazi tatu ngumu Simba

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. OFISA Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara amesema ana malengo matatu makubwa mbele yake, ambayo anatakiwa kuyatimiza msimu huu.

Barbara alisema malengo hayo ni kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu na bado wana mechi zaidi ya 20 hadi kumaliza msimu, lakini la pili ni kuifikisha timu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambalo tayari amelifikia.

“Jambo la tatu ambalo nimewekewa na natakiwa kulifikia ni kutetea ubingwa wa Kombe la Shirikisho (ASFC), ambalo tupo katika hatua ya pili na kwa jinsi ya kikosi chetu kilivyo bora hilo linawezekana,” alisema Barbara.

Katika hatua nyingine, Barbara alisema misimu miwili iliyopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika hawakufanya vizuri kwenye mechi za ugenini, lakini msimu huu mambo yatakuwa tofauti.

Alisema katika kuhakikisha ugenini wanakuwa na matokeo mazuri pia wamesajili wachezaji wenye uwezo wa kwenda kuipigania timu huko tofauti na misimu miwili iliyopita kikosi hakifanani na sasa.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz