Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barbara Gonzalez atua Cameroon, apanga kutumia fursa

Babra Azuiwa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez

Fri, 4 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Barbara Gonzalez, amekwenda nchini Cameroon na atahudhuria Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Senegal dhidi ya Misri itakayopigwa Februari 6 mwaka huu katika Dimba la Olembe nchini Cameroon.

Hatua hiyo inatokana na mwaliko kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika CAF, Patrice Motsepe.

Barbara ameondoka nchini hii leo, na klabu ya Simba imesema inataka kutumia fursa hiyo kudumisha uhusiano chanya baina ya klabu ya Simba, wadau na taasisi nyingine kubwa Barani Afrika zikiwemo za mpira wa miguu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live