Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza aichimba mkwara Simba

Ad784d67f5647d02f1029e370da96571 Baraza aichimba mkwara Simba

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Francis Baraza amesema Simba isitarajie mteremko katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kagera Sugar ambayo inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imejikusanyia pointi 27, itakuwa na kibarua kizito kuikabili Simba inayoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 52.

Akizungumza na gazeti hili leo, Baraza alisema anaiheshimu Simba kutokana na ubora wa kikosi chake ambacho kimesheheni wachezaji wazuri, lakini kwa maandalizi waliyoyafanya ana amini wanaenda kuondoka na pointi tatu nyumbani.

“Najua utakuwa mchezo mgumu wenye presha kubwa kwetu kutokana na aina ya timu tunayoenda kukutana nayo, tumetoka ugenini tumerudi na pointi mbili nyumbani naamini tunaenda kufanya vizuri,” alisema.

Kagera Sugar itashuka uwanjani katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu mbaya dhidi ya Simba, ambapo ilikubali kichapo cha mabao 2-0 katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Chanzo: www.habarileo.co.tz