Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza: Kusimama ligi kumenisaidia

Baraza Kageraa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Francis Baraza

Wed, 31 Aug 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Francis Baraza amefichua mapumziko ya Ligi Kuu yalivyomsaidia kujipanga upya ili kuboresha kikosi chake ambacho kinakabiliwa na majeruhi tangu kuanza kwa msimu huu.

Kocha huyo wa Kagera Sugar alisema alikuwa katika kipindi kigumu kwenye mechi mbili za awali baada ya nyota wake saba kuwa majeruhi.

“Ligi iliposimama nilishukuru. Japo sio wote ambao wataimarika, lakini baadhi yao wameanza kuimarika na kama watakuwa fiti, basi kwenye mechi ya Septemba 6 (dhidi ya Geita Gold) nitakuwa nao,” alisema Baraza.

Aliwataja baadhi ya wachezaji wake ambao ni majeruhi kuwa ni David Luhende ambaye aliumia akiwa kwenye timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Dickson Mhilu ambaye ameanza mazoezi kidogo kidogo na Edgar James.

“Huyu aliomba ruhusa aende kwao mara moja baada ya kuona hawezi kubaki Kagera peke yake wakati timu ikiwa imesafiri kwenye mechi zetu za awali,” alisema.

Aliwataja wengine kuwa ni Mpapi Nasibu ambaye amesema ni mchezaji aliyempa wakati mgumu kuwa nje ya uwanja wakati Ligi Kuu ilipoanza. “Mechi ziliposimama kupisha programu za Taifa Stars kwangu ilinisaidia kuboresha kikosi na wale ambao walikuwa hawapati nafasi ya kuanza kujaribu kuwatumia katika mazoezi na mechi kadhaa za kirafiki ikiwamo ya Kagera Combine.”

Chanzo: Mwanaspoti