Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baobab yaibutua Ceasiaa Queens WPL

Baobab Wins Baobab yaibutua Ceasiaa Queens WPL

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mabao mawili ya kipindi cha kwanza yameipa pointi tatu muhimu timu ya Baobab Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) dhidi ya Ceasiaa Queens ya mkoani Iringa.

Mchezo huo umepigwa jana katika dimba la Jamhuri Jijini Dodoma na kumalizika kwa Baobab kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kwa matokeo hayo timu hiyo imefikisha pointi 4 huku Ceasiaa Queens wakiwa hawana pointi yoyote.

Mchezo wa raundi ya kwanza uliofanyika katika dimba la Ilulu mkoani Lindi Baobab iliambulia pointi moja mara baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Amani Queens.

Ceasiaa Queens inapoteza kwa mara ya pili mfululizo mara baada ya mchezo wa kwanza kufungwa bao 1-0 na Alliance Girls mtanange uliofanyika katika dimba la Nyamagana Jijini Mwanza.

Mchezo huo ulianza taratibu kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu huku kukiwa na kosa kosa za hapa na pale.

Baobab ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 kupitia kwa mshambuliaji Jamila Rajabu kwa shuti kali mara baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Ceasiaa Queens Hadija Mohammed na Ever Wailes.

Dakika ya 26 almanusura mshambuliaji wa Ceasiaa,Janeth Matulanga aipatie timu yake bao lakini kipa wa Baobab Queens Hadija Mwita aliokoa na kuwa kona ambayo haikuwa na madhara yoyote.

Baobab ilijipatia bao la pili dakika ya 20 kupitia kwa winga Josephina Nyerenda kwa kichwa mara baada ya kuunganisha kona iliyopigwa na Annambez Lazaro.

Mshambuliaji hatari wa Ceasiaa Janeth Matulanga aliipatia timu yake bao dakika ya 44 kwa kichwa cha kuparaza kilichomshinda kipa wa Baobab Hadija Mwita.

Hadi mapumziko Baobab walikuwa mbele kwa mabao 2-1,kipindi Cha pili kilianza kwa kasi kwa Ceasiaa Queens kumtoa Christiana Chamwile na nafasi yake kuchukuliwa na Marry John.

Mabadiliko hayo yaliipa nguvu Ceasiaa lakini umakini wa kipa wa Baobab Jeanne Paulin uliisaidia timu yake kupata pointi tatu kutokana na kuokoa michomo ya washambuliaji Nasma Manduja na Janeth Matulanga.

Baobab ilimtoa Rahma Hassan na nafasi yake ikichukuliwa na Joyce Meshack lakini mabadiliko hayo hayakubalisha matokeo ya mchezo huo.

Hadi filimbi ya mwisho ya mwamuzi,Lilian Marwa kutoka Dar es salaam,Baobab Queens waliiibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo,Kocha wa Baobab Queens Juma Ikaba amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa kufuata maelekezo huku akikiri mchezo ulikuwa mgumu.

Kwa upande wake Kocha wa Ceasiaa Queens,Emmanuel Masawe amesema ameyapokea matokeo hayo na anaenda kujipanga kwa michezo inayofuata.

Chanzo: Mwanaspoti