Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baobab, Alliance hakuna mbabe WPL

WPL.jpeg Baobab, Alliance hakuna mbabe WPL

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kati ya Baobab Queens na Alliance Girl umemalizika jioni ya leo Jumatano Februari 15 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kwa timu hizo kutoka suluhu.

Licha ya timu hizo kushambuliana kwa zamu lakini hakuna timu iliyoweza kupata bao katika mchezo huo uliokuwa wa kufunga mzunguko wa kwanza wa ligi. Zifuatazo ni dondoo za mchezo huu.

Katika mabao 12 yaliyofungwa na Alliance Girls, mabao sita yamefungwa na Winfrida Charles ambaye katika mchezo wa leo ameshindwa kufunga kutokana na kubanwa vilivyo na mabeki wa Baobab Queens waliiongozwa na Neema John.

Beki wa Baobab, Neema Charles ameweka rekodi ya kucheza michezo yote ya mzunguko wa kwanza wa WPL (9) akicheza dakika 810.

Mchezo huo ulikuwa wa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ambapo jumla ya michezo miwili imechezwa, mwingine uliopigwa Uwanja wa Black Rhino, Karatu Tigers ikivaana na Fountain Gate Princess.

JKT Queens ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo katika ligi hiyo huku Mkwawa Queens ikiburuza mkia ikiwa haijashinda mchezo wowote na imefunga bao moja na kufungwa mabao 19.

Alliance imefikisha alama 14 ikiendelea kubaki katika nafasi tano huku Baobab ikifikisha pointi nane ikiendelea kubaki katika nafasi ya saba, Simba Queens inaongoza ikiwa na alama 22.

Alliance imefunga mabao 12 huku ikifungwa 14 na Baobab imefunga mabao nane na imefungwa 11. Katika michezo tisa iliyocheza Baobab imepoteza minne, imeshinda miwili na imetoa sare miwili. Alliance katika michezo tisa, imeshinda minne, imefungwa mitatu, imedroo miwili.

Chanzo: Mwanaspoti